Judges 2

Malaika Wa BWANA Huko Bokimu

Malaika wa BWANA akakwea kutoka Gilgali hadi Bokimu, naye akasema, “Niliwapandisha kutoka Misri na kuwaingiza katika nchi niliyoapa kuwapa baba zenu. Nikasema, ‘Kamwe sitalivunja Agano langu nanyi. Nanyi msifanye agano na watu wa nchi hii, bali mtazibomoa madhabahu zao.’ Lakini ninyi hamkunitii mimi. Kwa nini mmefanya jambo hili? Sasa basi ninawaambia kuwa sitawafukuza watoke katikati yenu ila watakuwa miiba kwenu, nao miungu yao itakuwa tanzi kwenu.”

Malaika wa BWANA alipomaliza kusema mambo haya kwa Waisraeli wote, watu wakalia kwa sauti kuu. Wakapaita mahali pale Bokimu. Nao wakamtolea BWANA sadaka.

Kifo Cha Yoshua

Baada ya Yoshua kuwapa watu ruhusa waende zao, Waisraeli wakaenda kwenye urithi wao wenyewe ili kumiliki nchi yao. Watu wakamtumikia BWANA siku zote za maisha za Yoshua na za wazee walioishi kuliko Yoshua, ambao walikuwa wameona mambo makuu ambayo BWANA alikuwa ametenda kwa ajili ya Israeli.

Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa akiwa na umri wa miaka 110. Wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-Heresi
2.9 Unajulikana pia kama Timnath-Sera, ona Yos 19:50; 24:30
katika nchi ya vilima ya Efraimu, kaskazini ya Mlima Gaashi.

10 Baada ya kizazi kile chote kukusanywa pamoja na baba zao, kikainuka kizazi kingine baada yao ambacho hakikumjua BWANA, wala matendo yale aliyokuwa ametenda kwa ajili ya Waisraeli. 11 Kwa hiyo Waisraeli wakatenda maovu machoni pa BWANA na kuwatumikia Mabaali. 12 Wakamwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyekuwa amewatoa katika nchi ya Misri. Wakaifuata na kuiabudu miungu mbalimbali ya mataifa yanayowazunguka. Wakamkasirisha BWANA, 13 kwa sababu walimwacha yeye na kutumikia Baali na Maashtorethi. 14 Hivyo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa wavamizi waliowateka nyara. Akawauza katika mikono ya adui zao pande zote, hivyo hawakuweza tena kuwazuia adui zao. 15 Po pote Israeli walipotoka kwenda kupigana, mkono wa BWANA ulikuwa kinyume nao ili kuwashinda, kama vile alivyokuwa amewaapia. Nao wakawa katika taabu kubwa.

16 Ndipo BWANA akawainua waamuzi, ambao waliwaokoa katika mikono ya hao watu waliowashambulia. 17 Lakini hawakuwasikiliza hata waamuzi wao, bali walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine na kuiabudu. Waligeuka mara na kuiacha njia ambayo baba zao waliiendea, yaani, njia ya kutii amri za BWANA. 18 Kila mara BWANA alipowainulia mwamuzi, BWANA alikuwa pamoja na huyo mwamuzi, naye aliwaokoa kutoka mikononi mwa adui zao kwa kipindi chote alichoishi yule mwamuzi. Kwa kuwa BWANA aliwahurumia kwa sababu ya kilio chao cha huzuni kwa ajili ya wale waliokuwa wakiwatesa na kuwataabisha. 19 Lakini kila mara mwamuzi alipokufa, watu walirudia katika hali mbaya ya uovu zaidi kuliko baba zao, wakiifuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu. Walikataa kuacha matendo yao maovu na njia zao za ukaidi.

20 Kwa hiyo BWANA akawakasirikia sana Israeli na kusema, “Kwa kuwa taifa hili limevunja Agano lile nililofanya na baba zao na hawakunisikiliza, 21 mimi nami sitafukuza taifa lo lote ambalo Yoshua aliliacha alipokufa. 22 Nitayatumia ili nipate kuwapima Israeli na kuona kama wataishika njia ya BWANA na kuenenda katika hiyo kama baba zao walivyofanya.” 23 BWANA alikuwa ameyaacha hayo mataifa yabaki; hakuyaondoa mara moja kwa kuyatia mikononi mwa Yoshua.

Copyright information for Neno