Leviticus 27

Kukomboa Kile Kilicho Cha BWANA

1BWANA akamwambia Mose, 2“Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Kama mtu ye yote ataweka nadhiri maalum ili kuweka watu wakfu kwa BWANA, kwa kutoa kiasi cha thamani inayolingana, 3thamani ya mwanaume mwenye kati ya umri wa miaka ishirini na miaka sitini atakombolewa kwa shekeli hamsini
27.3 Shekeli 50 za fedha ni sawa na gramu 600
za fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu;
4ikiwa ni mwanamke, weka thamani yake kwa shekeli thelathini
27.4 Shekeli 30 za fedha ni sawa na gramu 360
.
5Kama ni mwenye umri wa miaka kati ya mitano na ishirini, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli ishirini
27.5 Shekeli 20 za fedha ni sawa na gramu 240
, na mwanamke shekeli kumi
27.5 Shekeli 10 za fedha ni sawa na gramu 120
.
6Kama ni mtu mwenye umri kati ya mwezi mmoja na miaka mitano, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli tano za fedha, na ile ya mwanamke kuwa shekeli tatu
27.6 Shekeli tatu za fedha ni sawa na gramu 36
za fedha.
7Kama ni mtu mwenye miaka sitini na zaidi, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli kumi na tano
27.7 Shekeli 15 za fedha ni sawa na gramu 180
na mwanamke shekeli kumi.
8Kama mtu ye yote anayeweka nadhiri ni maskini mno kulipa kiasi kilichowekwa, atampeleka huyo mtu kwa kuhani, ambaye ataweka thamani yake kulingana na kile mweka nadhiri anachoweza kulipa.

9“ ‘Kama kile mtu alichokiwekea nadhiri ni mnyama anayekubalika kama sadaka kwa BWANA, mnyama wa namna hiyo aliyetolewa kwa BWANA anakuwa mtakatifu. 10Mtu haruhusiwi kumbadilisha au kutoa mnyama mzuri kwa mbaya, au mnyama mbaya kwa mzuri; kama atatoa mnyama badala ya mwingine, wanyama wote wawili, yaani yule aliyetolewa na yule aliyebadiliwa, huwa watakatifu. 11Kama alichokiwekea nadhiri ni mnyama aliye najisi kiibada, yaani yule asiye kubalika kuwa sadaka kwa BWANA, huyo mnyama lazima aletwe kwa kuhani, 12ambaye ataamua ubora wa mnyama huyo kama ni mzuri au mbaya. Thamani yo yote atakayoweka kuhani, hivyo ndivyo itakavyokuwa. 13Kama mwenye mnyama atapenda kumkomboa mnyama huyo, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake.

14“ ‘Kama mtu ataweka nyumba yake wakfu kama kitu kitakatifu kwa BWANA, kuhani ataamua ubora wa nyumba hiyo kama ni nzuri au mbaya. Thamani yo yote kuhani atakayoweka, basi hivyo ndivyo itakavyokuwa. 15Kama mtu aliyeweka nyumba yake wakfu ataikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nayo nyumba itakuwa tena yake.

16“ ‘Kama mtu anaweka sehemu ya ardhi ya jamaa yake wakfu kwa BWANA, thamani yake itawekwa kulingana na kiasi cha mbegu inayohitajiwa kupandwa katika ardhi hiyo, yaani homeri
27.16 Homeri moja ni sawa na efa 10, ambazo ni sawa na kilo 100
moja ya mbegu za shayiri kwa shekeli hamsini za fedha.
17Kama akiweka shamba lake wakfu katika Mwaka wa Yubile, ile thamani iliyokwisha wekwa itakuwa iyo hiyo. 18Lakini kama akiweka shamba lake wakfu baada ya Yubile, kuhani ataweka thamani kulingana na idadi ya miaka iliyobaki kufikia Mwaka unaofuata wa Yubile, na thamani yake iliyoamuliwa itapunguzwa. 19Kama mtu anayeweka wakfu shamba anataka kulikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nalo shamba litakuwa lake tena. 20Kama pengine halikomboi shamba, au kama ameliuza kwa mtu mwingine, kamwe haliwezi kukombolewa. 21Shamba litakapoachiwa mwaka wa Yubile, litakuwa takatifu, kama shamba lililotolewa kwa BWANA, nalo litakuwa mali ya makuhani.

22“ ‘Kama mtu ameweka wakfu kwa BWANA shamba alilonunua, ambalo si sehemu ya ardhi ya jamaa yake, 23kuhani ataamua thamani yake hadi Mwaka wa Yubile, naye huyo mtu atalazimika kulipa thamani yake siku hiyo kama kitu kitakatifu kwa BWANA. 24Katika Mwaka wa Yubile, shamba litarudishwa kwa mtu yule ambaye lilinunuliwa kutoka kwake, yule ambaye ardhi ilikuwa mali yake. 25Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu
27.25 Shekeli moja ya mahali patakatifu ni sawa na gramu 11
, gera
27.25 Gera ilikuwa sehemu ya ishirini ya shekeli
ishirini kwa shekeli.

26“ ‘Kwa vyo vyote, hakuna mtu atakayeweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa mnyama, kwa kuwa mzaliwa wa kwanza tayari ni mali ya BWANA; awe maksai au kondoo, ni wa BWANA. 27Kama ni mmoja wa wanyama walio najisi, aweza kumnunua kwa bei iliyowekwa, akiongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Kama hatamkomboa, mnyama huyo atauzwa kwa bei iliyowekwa.

28“ ‘Lakini cho chote kile mtu alichonacho na kukitoa kwa BWANA, ikiwa ni binadamu, au mnyama, au ardhi ya jamaa, chaweza kuuzwa au kukombolewa; cho chote kilichotolewa ni kitakatifu sana kwa BWANA.

29“ ‘Mtu ye yote aliyetolewa ili kuangamizwa, hawezi kukombolewa. Mtu kama huyo lazima auawe.

30“ ‘Zaka ya kila kitu kutoka shambani, ikiwa ni nafaka kutoka kwenye ardhi, au tunda kwenye miti, ni mali ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA. 31Kama mtu akikomboa cho chote cha zaka yake, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake. 32Zaka yote ya kundi la ng'ombe au la kondoo na mbuzi, kila mnyama wa kumi apitaye chini ya fimbo ya yule awachungaye, atakuwa mtakatifu kwa BWANA. 33Yule mnyama wa kumi hatachaguliwa kwa kigezo cha uzuri au ubaya, naye haruhusiwi kubadiliwa. Ikiwa atabadiliwa, basi mnyama yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa wote watahesabiwa kuwa watakatifu, na haiwezekani kuwakomboa.’ ”

34Haya ndiyo maagizo BWANA aliyompa Mose juu ya Mlima Sinai kwa ajili ya Waisraeli.

Copyright information for Neno