Nehemiah 3

Wajenzi Wa Ukuta

1Eliyashibu Kuhani Mkuu na makuhani wenzake walikwenda kufanya kazi na kulijenga upya Lango la Kondoo. Waliliweka wakfu na kuweka milango mahali pake, wakajenga hadi kufikia Mnara wa Mia Moja, ambao waliuweka wakfu hadi Mnara wa Hananeli. 2Watu wa Yeriko wakajenga sehemu zilizopakana nao, Zahuri mwana wa Imri aliendelea kujenga karibu nao.3Lango la Samaki lilijengwa upya na wana wa Hasena. Wakaweka boriti zake, wakaweka milango yake na makomeo na nondo. 4Meremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu iliyofuatia. Aliyemfuatia ni Meshulamu mwana wa Berekia, mwana wa Meshezabeli, alifanya ukarabati na aliyemfuatia ni Zadoki mwana wa Baana. 5Sehemu iliyofuatia ilikarabatiwa na watu kutoka Tekoa, lakini wakuu wao walikataa kufanya kazi chini ya wasimamizi wao.6Lango la Yeshana lilikarabatiwa na Yoyada mwana wa Pasea na Meshulamu mwana wa Besodeya. Wakaziweka boriti zake, milango, makomeo na nondo. 7Karibu nao ukarabati ulifanywa na watu kutoka Gibeoni na Mispa, Melati ya Gibeoni na Yadoni ya Meronothi, sehemu hizi zilikuwa chini ya mamlaka ya mtawala wa Ng'ambo ya Eufrati. 8Uzieli mwana wa Harhaya, mmoja wa masonara, walikarabati sehemu iliyofuatia na Hanania mmoja wa watengenezaji marashi, alikarabati sehemu iliyofuatia. Walitengeneza Yerusalemu mpaka kufikia Ukuta Mpana. 9Refaya mwana wa Huri, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia. 10Kupakana na sehemu hii, Yedaya mwana wa Harumafu alikarabati sehemu iliyokuwa mkabala na nyumba yake, naye Hatushi mwana wa Hashabnea alifanya ukarabati sehemu iliyofuatia. 11Malkiya mwana wa Harimu na Hashubu mwana wa Pahath-Moabu walikarabati sehemu nyingine pamoja na Mnara wa Matanuru. 12Shalumu mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia akisaidiana na binti zake.13Lango la Bondeni lilikarabatiwa na Hanuni na wakazi wa Zanoa. Walilijenga kwa upya na kuweka milango yake na makomeo na nondo mahali pake. Pia walikarabati ukuta wenye urefu wa mita 450 hadi Lango la Samadi.14Lango la Samadi lilikarabatiwa na Malkiya mwana wa Rekabu, mtawala wa wilaya ya Beth-Hakeremu. Alijenga kwa upya na kuweka milango yake makomeo na nondo.15Lango la Chemchemi lilikarabatiwa na Shalumu mwana wa Kolhoze, mtawala wa wilaya ya Mispa. Alilijenga kwa upya, akaliezeka na kuweka milango yake, makomeo yake na nondo mahali pake. Pia alikarabati ukuta wa Bwawa la Siloamu karibu na Bustani ya Mfalme hadi kwenye ngazi zinazoshuka kutoka Mji wa Daudi. 16Sehemu iliyofuatia, Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-Zuri, alikarabati kufikia mkabala na makaburi ya Daudi, mpaka kwenye bwawa lililotengenezwa na kufikia Nyumba ya Mashujaa.

17Sehemu iliofuatia, ukarabati ulifanywa na Walawi chini ya uongozi wa Rehumu mwana wa Bani. Aliyefuatia ni Hashabia, mtawala wa nusu ya wilaya ya Keila. Aliendeleza ukarabati katika sehemu inayohusu wilaya yake. 18Sehemu iliofuatia, ukarabati ulifanywa na ndugu zao chini ya usimamizi wa Binui, mwana wa Henadadi, mtawala wa nusu ya wilaya ya Keila. 19Sehemu iliofuatia, Ezeri mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia ile sehemu inayotazamana na mwinuko wa kuelekea kwenye ghala la kuhifadhia silaha, mpaka kwenye pembe ya ukuta. 20Sehemu iliofuatia, Baruki mwana wa Zabai alikarabati kwa bidii sehemu nyingine kuanzia ile pembe mpaka kwenye lango la nyumba ya Eliyashibu Kuhani Mkuu. 21Sehemu iliofuatia, Meremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia penye lango la nyumba ya Eliyashibu mpaka mwisho wake.

22Sehemu iliofuatia, ukarabati ulifanywa na makuhani kuanzia eneo lililouzunguka mji. 23Baada yao Benyamini na Hashubu walikarabati mbele ya nyumba zao, baada yao Azaria mwana wa Maaseya, mwana wa Anania alifanya ukarabati kando ya nyumba yake. 24Sehemu iliofuatia, Binui mwana wa Henadadi alikarabati sehemu nyingine, kuanzia kwenye nyumba ya Azaria mpaka kwenye pembe ya ukuta. 25Naye Palali, mwana wa Uzai alijenga sehemu iliyokuwa mkabala na pembe ya ukuta mpaka kwenye mnara wa juu ambao unajitokeza kuanzia kwenye jumba la kifalme kando ya ua wa walinzi. Sehemu iliofuatia, Pedaya mwana wa Paroshi, 26na watumishi wa Hekalu waishio juu ya kilima cha Ofeli walikarabati hadi kufikia mkabala na Lango la Maji, kuelekea mashariki pamoja na ule mnara uliojitokeza. 27Sehemu iliofuatia, watu wa Tekoa walikarabati sehemu nyingine, kuanzia mnara mkubwa utokezao hadi ukuta wa Ofeli.28Makuhani walifanya ukarabati juu ya Lango la Farasi, kila mmoja mbele ya nyumba yake. 29Baada yao, Sadoki mwana wa Imeri alifanya ukarabati mkabala na nyumba yake. Sehemu iliofuatia, Shemaya mwana wa Shekania, mlinzi wa Lango la Mashariki, alifanya ukarabati. 30Sehemu iliofuatia, Hanania mwana wa Shelemia na Hanuni, mwana wa sita wa Salafu, alikarabati sehemu nyingine. Baada yao, Meshulamu mwana wa Berekia alikarabati sehemu iliyokuwa mkabala na nyumba zake za kuishi. 31Sehemu iliofuatia, Malkiya, mmoja wa masonara, alifanya ukarabati mpaka kwenye nyumba za Wanethini
3.31 Yaani watumishi wa Hekalu
na wafanyabiashara, mkabala na Lango la Ukaguzi, hadi kufikia chumba kilicho juu ya pembe.
32Masonara na wafanya biashara walifanya ukarabati kati ya chumba kilichoko juu ya pembe ya Lango la Kondoo.

Copyright information for Neno