Numbers 26

Kuhesabiwa Watu Mara Ya Pili

1Baada ya hiyo tauni, BWANA akamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni, 2“Hesabu jumuiya yote ya Kiisraeli kwa jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao wanaweza kutumika katika jeshi la Israeli.” 3Hivyo Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ng'ambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema, 4“Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama BWANA alivyomwagiza Mose.”Hawa ndio Waisraeli waliotoka Misri:

5Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa:
 • kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki;
 • kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu;
6kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahezroni; kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi. 7Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.

8Mwana wa Palu alikuwa Eliabu, 9nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Mose na Aroni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walipomwasi BWANA. 10Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume 250. Nao walikuwa kama alama ya onyo. 11Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa.12Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa:
 • kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli;
 • kutoka kwa Yamini, ukoo wa Wayamini;
13kutoka kwa Sohari, ukoo wa Wasohari; kutoka kwa Shauli, ukoo wa Washauli. 14Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa 22,200.15Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa:
 • kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni;
 • kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi;
 • kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni;
16kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni; kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri; 17kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi; kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli. 18Hizi ndizo zilizokuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa 40,500.19Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani.

20Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa:
 • kutoka kwa Shela, ukoo wa Washela;
 • kutoka kwa Peresi, ukoo wa Waperesi;
 • kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera.
21Wazao wa Peresi walikuwa: kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahezroni; kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli. 22Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa 76,500.23Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa:
 • kutoka kwa Tola, ukoo wa Watola;
 • kutoka kwa Pua, ukoo wa Wapua;
24kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu; kutoka kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni. 25Hizi ndizo zilizokuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa 64,300.26Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa:
 • kutoka kwa Seredi, ukoo wa Waseredi;
 • kutoka kwa Eloni, ukoo wa Waeloni;
 • kutoka kwa Yahleeli, ukoo wa Wayaleeli.


27Hizi ndizo zilizokuwa koo za Zabuloni, wale waliohesabiwa walikuwa 60,500.28Wazao wa Yosefu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa:

29Wazao wa Manase:
 • kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi);
 • kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi.
30Hawa ndio waliokuwa wazao wa Gileadi: kutoka kwa Iezeri, ukoo wa Waiezeri; kutoka kwa Heleki, ukoo wa Waheleki; 31kutoka kwa Asrieli, ukoo wa Waasrieli; kutoka kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu; 32kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida; kutoka kwa Heferi, ukoo wa Waheferi. 33(Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.) 34Hizi ndizo zilizokuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa 52,700.35Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao:
 • kutoka kwa Shuthela, ukoo wa Washuthela;
 • kutoka kwa Bekeri, ukoo wa Wabekeri;
 • kutoka kwa Tahani, ukoo wa Watahani;
36Hawa ndio walikuwa wazao wa Shuthela: kutoka kwa Erani, ukoo wa Waerani. 37Hizi ndizo zilizokuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa 32,500.Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yosefu kwa koo zao.38Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa:
 • kutoka kwa Bela, ukoo wa Wabela;
 • kutoka kwa Ashbeli, ukoo wa Waashbeli;
 • kutoka kwa Ahiramu, ukoo wa Waahiramu;
39kutoka kwa Shufamu, ukoo wa Washufamu; kutoka kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu. 40Wazao wa Bela kutoka kwa Ardi na Naamani walikuwa: kutoka kwa Ardi, ukoo wa Waardi; kutoka kwa Naamani, ukoo wa Wanaamani. 41Hizi ndizo zilizokuwa koo za Benyamini; wale waliohesabiwa walikuwa 45,600.42Hawa ndio waliokuwa wazao wa Dani kwa koo zao:
 • kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu.


Hizi ndizo zilizokuwa koo za Dani:
43Wote walikuwa koo za Washuhamu; wale waliohesabiwa walikuwa 64,400.44Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa:
 • kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna;
 • kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi;
 • kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia;
45kutoka kwa wazao wa Beria: kutoka kwa Heberi, ukoo wa Waheberi; kutoka kwa Malkieli, ukoo wa Wamalkieli. 46(Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.) 47Hizi ndizo zilizokuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa 53,400.48Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa:
 • kutoka kwa Yahseeli, ukoo wa Wayaseeli;
 • kutoka kwa Guni, ukoo wa Waguni;
49kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri; kutoka kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu. 50Hizi ndizo zilizokuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa 45,400.51Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa 601,730.52BWANA akamwambia Mose, 53“Watagawiwa nchi kama urithi kwa kulingana na hesabu ya majina. 54Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa. 55Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao. 56Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.”57Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao:
 • kutoka kwa Gershoni, ukoo wa Wagerishoni;
 • kutoka kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi;
 • kutoka kwa Merari, ukoo wa Wamerari.
58Hizi pia zilikuwa koo za Walawi: ukoo wa Walibni; ukoo wa Wahebroni; ukoo wa Wamatili; ukoo wa Wamushi; ukoo wa Wakora. (Kohathi alikuwa baba aliyemzaa Amramu; 59jina la mke wa Amramu ni Yokobedi, naye pia alikuwa mzao wa Lawi, ambaye alizaliwa kwa Walawi nchini Misri. Alimzalia Amramu: Aroni, Mose na dada yao Miriamu. 60Aroni alikuwa baba yake Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari. 61Lakini Nadabu na Abihu walikufa wakati walipotoa sadaka mbele za BWANA kwa moto usioruhusiwa.)62Wanaume wote wa Walawi wa umri wa mwezi mmoja na zaidi walikuwa 23,000. Wao hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu hawakupokea urithi miongoni mwao.63Hawa ndio walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari wakati walipowahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ng'ambo ya Yeriko. 64Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Mose na kuhani Aroni wakati walipowahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai. 65Kwa maana BWANA alikwishawaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.

Copyright information for Neno