Numbers 29

Sikukuu Ya Tarumbeta

“ ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu na msifanye kazi ya kawaida. Ni siku kwa ajili yenu ya kupiga tarumbeta. Mtatayarisha sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri impendezayo BWANA ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. Pamoja na fahali andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume, andaa unga sehemu ya kumi mbili za efa; na pamoja na wana-kondoo saba kila mmoja aandaliwe na sehemu ya kumi ya efa ya unga. Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi kufanya upatanisho kwa ajili yenu. Hivi ni nyongeza ya sadaka za kuteketezwa kila mwezi na kila siku pamoja na sadaka zake za nafaka na sadaka za vinywaji kama ilivyoainishwa. Ni sadaka zinazotolewa kwa BWANA kwa moto, harufu inayopendeza.

Siku Ya Upatanisho

“ ‘Kwenye siku ya kumi ya mwezi huu wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu. Mtajikana wenyewe na msifanye kazi. Toeni sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza BWANA. Pamoja na fahali andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini; 10 na kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba andaa sehemu ya kumi ya unga laini kwa kila mmoja. 11 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho, na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka zake za vinywaji.

Sikukuu Ya Vibanda

12 “ ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Adhimisheni sikukuu kwa BWANA kwa siku saba. 13 Toeni sadaka ya kuteketezwa mafahali wachanga kumi na watatu, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza BWANA. 14 Pamoja na hao mafahali kumi na watatu, kila mmoja aandaliwe na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo waume wawili, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini; 15 na kwa wana-kondoo kumi na wanne, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi ya efa ya unga laini. 16 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka ya vinywaji.

17 “ ‘Katika siku ya pili andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 18 Pamoja na mafahali, kondoo waume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 19 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

20 “ ‘Katika siku ya tatu andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 21 Pamoja na mafahali, kondoo waume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 22 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

23 “ ‘Katika siku ya nne andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 24 Pamoja na mafahali, kondoo waume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 25 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

26 “ ‘Katika siku ya tano andaeni mafahali tisa, kondoo waume wawili na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 27 Pamoja na mafahali, kondoo waume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za kinywaji kulingana na idadi iliyoainishwa. 28 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi katika nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka pamoja na sadaka ya kinywaji.

29 “ ‘Katika siku ya sita andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 30 Pamoja na mafahali, kondoo waume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 31 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

32 “ ‘Katika siku ya saba andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo waume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 33 Pamoja na mafahali, kondoo waume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 34 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

35 “ ‘Katika siku ya nane mtakuwa na kusanyiko, na msifanye kazi ya kawaida. 36 Toeni sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri inayompendeza BWANA, sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo waume saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 37 Pamoja na fahali, kondoo dume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka, na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 38 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka pamoja na sadaka ya kinywaji.

39 “ ‘Zaidi ya kile unachoweka nadhiri na sadaka zenu za hiari, andaeni hizi kwa ajili ya BWANA kwenye sikukuu zenu zilizoamuriwa: sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za nafaka, sadaka za vinywaji, pamoja na sadaka zenu za amani.’ ”

40 Mose akawaambia Waisraeli yale yote BWANA aliyomwagiza.

Copyright information for Neno