Numbers 34

Mipaka Ya Kanaani

1BWANA akamwambia Mose, 2“Waamuru Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia nchi ya Kanaani, nchi ambayo itagawanywa kwenu kama urithi itakuwa na mipaka ifuatayo:

3“ ‘Upande wenu wa kusini utajumuisha sehemu ya Jangwa la Sini kufuata mpaka wa Edomu. Upande wa mashariki mpaka wenu wa kusini utaanzia mwisho wa Bahari ya Chumvi
34:3 Yaani Bahari Mfu
,
4katiza kusini mwa Pito la Akrabimu, endelea mpaka Sini na kwenda kusini ya Kadesh-Barnea. Kisha mpaka huo utaenda hadi Hasar-Adari hadi Azmoni, 5mahali ambapo utapinda, na kuunganika na mpaka wa Misri na kumalizikia kwenye Bahari ya Kati
34:5 Yaani Mediterania
.

6“ ‘Mpaka wenu wa magharibi utakuwa Bahari ya Kati. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa magharibi.

7“ ‘Kwa mpaka wenu wa kaskazini, wekeni alama kuanzia Bahari ya Kati hadi mlima Hori, 8na kutoka mlima Hori hadi Pito la Hamathi. Kisha mpaka utaenda hadi Sedadi, 9kuendelea hadi Zifroni, na kuishia Hazar-Enani. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa kaskazini.

10“ ‘Kwa mpaka wenu wa mashariki, wekeni alama kuanzia Hazar-Enani hadi Shefamu. 11Mpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye mitelemko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi
34:11 Yaani Bahari ya Galilaya
.
12Kisha mpaka utashuka kuelekea Mto Yordani na kuishia katika Bahari ya Chumvi.

“ ‘Hii itakuwa nchi yenu, ikiwa na mipaka yake kila upande.’ ”

13Mose akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi. BWANA ameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu, 14kwa sababu jamaa ya kabila la Reubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase wamekwishapokea urithi wao. 15Haya makabila mawili na nusu wamekwishapokea urithi wao upande wa mashariki wa Yordani ng'ambo ya Yeriko, kuelekea maawio ya jua.”

16BWANA akamwambia Mose, 17“Haya ndiyo majina ya watu ambao watakusaidia kugawanya nchi kama urithi: Eleazari kuhani na Yoshua mwana wa Nuni. 18Tena uteue kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia kuigawanya nchi. 19Haya ndiyo majina yao:
  • “Kalebu mwana wa Yefune,
  • kutoka kabila la Yuda;
20Shemueli mwana wa Amihudi, kutoka kabila la Simeoni; 21Elidadi mwana wa Kisloni, kutoka kabila la Benyamini; 22Buki mwana wa Yogli, kiongozi kutoka kabila la Dani; 23Hanieli mwana wa Efodi, kiongozi kutoka kabila la Manase mwana wa Yosefu; 24Kemueli mwana wa Shiftani, kiongozi kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yosefu; 25Elisafani mwana wa Parnaki, kiongozi kutoka kabila la Zabuloni; 26Patieli mwana wa Azani, kiongozi kutoka kabila la Isakari; 27Ahihudi mwana wa Shelomi, kiongozi kutoka kabila la Asheri; 28Pedaheli mwana wa Amihudi, kiongozi kutoka kabila la Naftali.” 29Hawa ndio watu ambao BWANA aliamuru kuwa wagawanye urithi kwa Waisraeli katika nchi ya Kanaani.

Copyright information for Neno