Numbers 7

Sadaka Wakati Wa Kuweka Wakfu Maskani Ya BWANA

Mose alipomaliza kuisimamisha Maskani, aliitia mafuta na kuiweka wakfu pamoja na samani zake zote. Pia alitia madhabahu mafuta na kuweka wakfu pamoja na vyombo vyake vyote. Ndipo viongozi wa Israeli, wale wakuu wa jamaa waliokuwa viongozi wa kabila wasimamizi wa wale waliohesabiwa, wakatoa sadaka. Walizileta kama matoleo yao mbele za BWANA: magari sita ya kukokotwa yaliyofunikwa, pamoja na maksai kumi na wawili; yaani maksai mmoja kutoka kwa kila kiongozi, na gari moja la kukokotwa kutoka kwa kila viongozi wawili. Haya waliyaleta mbele ya Maskani.

BWANA akamwambia Mose, “Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Kukutania. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.”

Hivyo Mose akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai, na kuwapa Walawi. Aliwapa Wagerishoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao, na pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Aroni. Lakini Mose hakuwapa Wakohathi cho chote kati ya hivyo, kwa sababu walitakiwa kubeba vitu vitakatifu mabegani mwao, vile walikuwa wanawajibika.

10 Wakati madhabahu ilipotiwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu. 11 Kwa maana BWANA alikuwa amemwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.”12 Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni, mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda.

13 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130
7.13 Shekeli 130 za fedha ni sawa na kilo 1.5
, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini
7.13 Shekeli 70 za fedha ni sawa gramu 800
, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;
14 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi
7.14 Shekeli 10 za dhahabu ni sawa na gramu 110
, likiwa limejazwa uvumba;
15 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 16 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 17 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.18 Siku ya pili yake Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa kabila la Isakari, alileta sadaka yake.

19 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 20 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 21 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 22 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 23 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari.24 Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa kabila la Zabuloni, alileta sadaka yake.

25 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 26 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 27 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 28 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 29 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni.30 Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, kiongozi wa kabila la Reubeni, alileta sadaka yake.

31 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 32 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 33 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 34 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 35 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Elisuri mwana wa Shedeuri.36 Siku ya tano Shelumieli mwana wa Surishadai, kiongozi wa watu wa Simeoni, alileta sadaka yake.

37 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 38 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 39 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 40 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 41 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Shelumieli mwana wa Surishadai.42 Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, kiongozi wa watu wa Gadi, alileta sadaka yake.

43 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 44 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 45 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 46 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 47 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Eliasafu mwana wa Deueli.48 Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu, alileta sadaka yake.

49 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 50 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 51 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 52 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 53 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Elishama mwana wa Amihudi.54 Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, kiongozi wa watu wa Manase, alileta sadaka yake.

55 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 56 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 57 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 58 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 59 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.60 Siku ya tisa Abidani mwana wa Gideoni, kiongozi wa watu wa Benyamini, alileta sadaka yake.

61 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 62 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 63 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 64 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 65 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Abidani mwana wa Gideoni.66 Siku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, kiongozi wa watu wa Dani, alileta sadaka yake.

67 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 68 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 69 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 70 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 71 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Ahiezeri mwana wa Amishadai.72 Siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, kiongozi wa watu wa Asheri, alileta sadaka yake.

73 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 74 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 75 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 76 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 77 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.78 Siku ya kumi na mbili Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa watu wa Naftali, alileta sadaka yake.

79 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 80 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 81 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 82 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 83 maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Ahira mwana wa Enani.84 Hizi zilikuwa ndizo sadaka za viongozi wa Israeli madhabahu ilipowekwa wakfu wakati ilipotiwa mafuta: sahani kumi na mbili za fedha, bakuli kumi na mbili za fedha za kunyunyizia, na masinia kumi na mawili ya dhahabu. 85 Kila sahani ya fedha ilikuwa na uzito wa shekeli 130, na kila bakuli la fedha la kunyunyizia lilikuwa na uzito wa shekeli sabini. Masinia yote kumi na mawili yalikuwa na uzito wa shekeli 2,400
7.85 Shekeli 2,400 za fedha ni sawa na kilo 28
kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.
86 Sahani kumi na mbili za dhahabu zilizojazwa uvumba zilikuwa na uzito wa shekeli kumi kila moja, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Kwa jumla, sahani za dhahabu zilikuwa na uzito wa shekeli 120
7.86 Shekeli 120 za dhahabu ni sawa na kilo 1.4
.
87 Jumla ya wanyama waliotolewa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa walikuwa fahali kumi na wawili wachanga, kondoo waume kumi na wawili na wana-kondoo waume kumi na wawili wa mwaka mmoja, pamoja na sadaka zao za nafaka. Mbuzi waume kumi na wawili walitolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi. 88 Jumla ya wanyama kwa ajili ya dhabihu ya sadaka ya amani walikuwa maksai ishirini na wanne, kondoo waume sitini, mbuzi waume wa mwaka mmoja sitini na wana-kondoo waume wa mwaka mmoja sitini. Hizi zilikuwa ndizo sadaka zilizoletwa kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu baada ya kutiwa mafuta.

89 Mose alipoingia kwenye Hema la Kukutania kuzungumza na BWANA, alisikia sauti ikisema naye kutoka kati ya wale makerubi wawili waliokuwa juu ya kile kiti cha rehema, juu ya Sanduku la Ushuhuda. Mose akazungumza naye.

Copyright information for Neno