Psalms 1

KITABU CHA KWANZA

Zaburi 1-41

Furaha Ya Kweli

1Heri mtu yule ambaye
haendi katika shauri la watu waovu,
wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi
au kuketi katika baraza la wenye mizaha.
2Bali huifurahia sheria ya BWANA,
naye huitafakari hiyo sheria mchana na usiku.
3Mtu huyo ni kama mti uliopandwa
kando ya vijito vya maji,
ambao huzaa matunda kwa majira yake
na majani yake hayanyauki.
Lo lote afanyalo hufanikiwa.

Huzuni Ya Waovu

4Sivyo walivyo waovu!
Wao ni kama makapi
yapeperushwayo na upepo.
5Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,
wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
6Kwa maana BWANA huziangalia njia za mwenye haki,
bali njia ya waovu itaangamia.
Copyright information for Neno