Psalms 110

BWANA Na Mfalme Wake Mteule

(Zaburi Ya Daudi)

1BWANA amwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
mpaka nitakapowafanya adui zako
kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
2BWANA ataeneza fimbo yako ya utawala
yenye nguvu kutoka Sayuni;
utatawala katikati ya adui zako.
3Askari wako watajitolea kwa moyo
katika siku yako ya vita.
Ukiwa umevikwa fahari takatifu,
kutoka kwenye tumbo la mapambazuko
utapokea umande wa ujana wako
110.3 Au: vijana wako watakujia kama umande
.
4BWANA ameapa,
naye hatabadilisha mawazo yake:
“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”
5Bwana yuko mkono wako wa kuume,
atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
6Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga
na kuwaponda watawala wa dunia nzima.
7Atakunywa maji katika kijito kando ya njia
110.7 Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka
,
kwa hiyo atainua kichwa chake juu.
Copyright information for Neno