Psalms 117

Sifa Za BWANA

1Msifuni BWANA, enyi mataifa yote;
mtukuzeni yeye, enyi watu wote.
2Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu,
uaminifu wa BWANA unadumu milele.
Msifuni BWANA.
Copyright information for Neno