Psalms 2

Mfalme Aliyechaguliwa Na Mungu

1Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya,
na mataifa kula njama bure?
2Wafalme wa dunia wanajipanga
na watawala wanajikusanya pamoja
dhidi ya BWANA
na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.
3Wanasema, “Tuvunje minyororo yao
na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”
4Yeye atawalaye mbinguni hucheka,
Bwana huwadharau.
5Kisha huwakemea katika hasira yake
na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,
6“Nimemtawaza mfalme wangu
juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”

Ushindi Wa Mfalme

7Nitatangaza amri ya BWANA:
Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu,
leo mimi nimekuzaa.
8Niombe, nami nitayafanya mataifa
kuwa urithi wako,
miisho ya dunia kuwa milki yako.
9Utawatawala kwa fimbo ya kifalme ya chuma
na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”
10Kwa hiyo, ninyi wafalme, iweni na hekima;
mwonyeke, enyi watawala wa dunia.
11Mtumikieni BWANA kwa hofu
na mshangilieni kwa kutetemeka.
12Mbusu Mwana, asije akakasirika
nawe ukaangamizwa katika njia yako,
kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula.
Heri wote wanaomkimbilia.
Copyright information for Neno