Psalms 8

Utukufu Wa Mungu Na Heshima Ya Mwanadamu

(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Gitithi. Zaburi Ya Daudi)

1Ee BWANA, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Umeuweka utukufu wako
juu ya mbingu.
2Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao
umeweka sifa,
kwa sababu ya watesi wako,
kuwanyamazisha adui na mlipiza kisasi.
3Nikiziangalia mbingu zako,
kazi ya vidole vyako,
mwezi na nyota,
ulizoziratibisha,
4mwanadamu ni kitu gani hata umkumbuke,
binadamu hata umwangalie?
5Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu,
umemvika taji ya utukufu na heshima.
6Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako;
umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
7Kondoo, mbuzi na ng'ombe wote pia,
naam, na wanyama wa kondeni,
8ndege wa angani na samaki wa baharini,
naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari.
9Ee BWANA, Bwana wetu,
tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Copyright information for Neno