Psalms 95

Wimbo Wa Kumsifu Mungu

1Njoni, tumwimbie BWANA kwa furaha;
tumfanyie kelele za shangwe
Mwamba wa wokovu wetu.
2Tuje mbele zake kwa shukrani,
tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.
3Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu,
mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4Mkononi mwake mna vilindi vya dunia
na vilele vya milima ni mali yake.
5Bahari ni yake, kwani ndiye aliyeifanya,
na mikono yake iliumba nchi kavu.
6Njoni, tusujudu tumwabudu,
tupige magoti mbele za BWANA Muumba wetu,
7kwa maana yeye ndiye Mungu wetu
na sisi ni watu wa malisho yake,
kondoo chini ya utunzaji wake.
Kama mkiisikia sauti yake, leo,
8msiifanye migumu mioyo yenu
kama mlivyofanya kule Meriba
95.8 Meriba maana yake ni Kugombana
,
kama mlivyofanya siku ile
kule Masa
95.8 Masa maana yake ni Kujaribiwa
jangwani,
9ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima,
ingawa walikuwa wameyaona niliyoyafanya.
10Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile,
nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka,
nao hawajazifahamu njia zangu.”
11Kwa hiyo nikaapa katika hasira yangu,
“Kamwe hawataingia rahani mwangu.”
Copyright information for Neno