Psalms 100

Dunia Yote Yaitwa Kumsifu Mungu

(Zaburi Ya Shukrani)

Mpigieni BWANA kelele za shangwe,
dunia yote.
Mwabuduni BWANA kwa furaha;
njoni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.
Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu.
Yeye ndiye aliyetuumba,
sisi tu mali yake;
sisi tu watu wake,
kondoo wa malisho yake.
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani
na katika nyua zake kwa kusifu,
mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
Kwa maana BWANA ni mwema
na upendo wake wadumu milele;
uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.
Copyright information for Neno