Psalms 11

Kumtumaini BWANA

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)

Kwa BWANA ninakimbilia,
unawezaje basi kuniambia:
“Ruka kama ndege kwenye mlima wako.
Hebu tazama, waovu wanapinda pinde zao,
huweka mishale kwenye uzi wake,
wakiwa gizani ili kuwapiga
wanyofu wa moyo.
Wakati misingi imeharibiwa,
mwenye haki anaweza kufanya nini?”
BWANA yuko ndani ya Hekalu lake takatifu;
BWANA yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni.
Huwaangalia wana wa watu,
macho yake yanawajaribu.
BWANA huwajaribu wenye haki,
lakini waovu na wale wanaopenda jeuri
nafsi yake huwachukia.
Juu ya waovu atawanyeshea makaa ya moto mkali
na kiberiti kinachowaka,
upepo wenye joto kali ndio fungu lao.
Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki,
hupenda haki;
watu wanyofu watauona uso wake.
Copyright information for Neno