Psalms 114

Maajabu Ya Mungu Wakati Israeli Walipotoka Misri

Wakati Israeli walipotoka Misri,
nyumba ya Yakobo
kutoka kwa watu wa lugha ngeni,
Yuda akawa makao matakatifu ya Mungu,
Israeli akawa milki yake.
Bahari ilitazama ikakimbia,
Yordani ulirudi nyuma,
milima ilirukaruka kama kondoo waume,
vilima kama wana-kondoo.
Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia,
Ee Yordani, nawe ukarudi nyuma,
enyi milima mkarukaruka kama kondoo waume,
enyi vilima, kama wana-kondoo?
Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana,
mbele za Mungu wa Yakobo,
yeye aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji,
mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.
Copyright information for Neno