Psalms 120

Kuomba Msaada

(Wimbo Wa Kwenda Juu)

Katika dhiki yangu namwita BWANA,
naye hunijibu.
Ee BWANA, uniokoe kutoka midomo ya uongo
na ndimi za udanganyifu.
Atakufanyia nini,
au akufanyie nini zaidi,
Ewe ulimi mdanganyifu?
Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa,
kwa makaa yanayowaka
ya mti wa mretemu.
Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki,
kwamba naishi katikati
ya hema za Kedari!
Nimeishi muda mrefu mno
miongoni mwa wale
wanaochukia amani.
Mimi ni mtu wa amani;
lakini ninaposema,
wao wanataka vita.
Copyright information for Neno