Psalms 123

Kuomba Rehema

(Wimbo Wa Kwenda Juu)

Ninayainua macho yangu kwako,
kwako wewe ambaye
kiti cha enzi kiko mbinguni.
Kama vile macho ya watumwa
yatazamavyo mkono wa bwana wao,
kama vile macho ya mtumishi wa kike
yatazamavyo mkono wa bibi yake,
ndivyo macho yetu yamtazamavyo BWANA Mungu wetu,
mpaka atakapotuhurumia.
Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu,
kwa maana tumevumilia dharau nyingi.
Tumevumilia dhihaka nyingi
kutoka kwa wenye kiburi,
dharau nyingi
kutoka kwa wenye majivuno.
Copyright information for Neno