Psalms 125

Usalama Wa Watu Wa Mungu

(Wimbo Wa Kwenda Juu)

Wale wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,
ambao hauwezi kutikisika wadumu milele.
Kama milima inavyozunguka Yerusalemu,
ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake
sasa na hata milele.
Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi
waliopewa wenye haki,
ili kwamba wenye haki wasije
wakatumia mikono yao
kutenda ubaya.
Ee BWANA, watendee mema walio wema,
wale walio wanyofu wa moyo.
Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka,
BWANA atawafukuza
pamoja na watenda mabaya.
Amani iwe juu ya Israeli.
Copyright information for Neno