Psalms 126

Kurejeshwa Kutoka Utumwani

(Wimbo Wa Kwenda Juu)

BWANA alipowarejeza mateka Sayuni,
tulikuwa kama watu walioota ndoto.
Vinywa vyetu vilijaa kicheko,
ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.
Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,
“BWANA amewatendea mambo makuu.”
BWANA ametutendea mambo makuu,
nasi tumejaa furaha.
Ee BWANA, turejeshee watu wetu waliotekwa,
kama vijito katika Negebu.
Wapandao kwa machozi
watavuna kwa nyimbo za shangwe.
Yeye azichukuaye mbegu zake
kwenda kupanda,
huku akilia,
atarudi kwa nyimbo za shangwe,
akiwa ameyachukua
matita ya mavuno yake.
Copyright information for Neno