Psalms 127

Bila Mungu, Kazi Ya Mwanadamu Haifai

(Wimbo Wa Kwenda Juu. Wa Solomoni)

BWANA asipoijenga nyumba,
wajengao hufanya kazi bure.
BWANA asipoulinda mji,
walinzi wakesha bure.
Mnajisumbua bure kuamka mapema
na kuchelewa kulala,
mkitaabikia chakula:
kwa maana yeye huwapa usingizi
wapenzi wake.
Wana ni urithi utokao kwa BWANA,
watoto ni zawadi kutoka kwake.
Kama mishale mikononi mwa shujaa
ndivyo walivyo wana
awazaao mtu katika ujana wake.
Heri mtu ambaye podo lake
limejazwa nao.
Hawataaibishwa wanaposhindana
na adui zao langoni.
Copyright information for Neno