Psalms 128

Thawabu Ya Kumtii BWANA

(Wimbo Wa Kwenda Juu)

Heri ni wale wote wamchao BWANA,
waendao katika njia zake.
Utakula matunda ya kazi yako;
baraka na mafanikio vitakuwa vyako.
Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao
katika nyumba yako;
wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni
kuizunguka meza yako.
Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa
mtu amchaye BWANA.
BWANA na akubariki kutoka Sayuni
siku zote za maisha yako,
na uone mafanikio ya Yerusalemu,
nawe ujaliwe kuishi
uone watoto wa watoto wako.
Amani iwe juu ya Israeli.
Copyright information for Neno