Psalms 13

Sala Ya Kuomba Msaada

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)

Mpaka lini, Ee BWANA? Je, utanisahau milele?
Utanificha uso wako mpaka lini?
Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini
na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu?
Adui zangu watanishinda mpaka lini?
Nitazame unijibu, Ee BWANA Mungu wangu.
Uyatie nuru macho yangu,
ama sivyo nitalala usingizi wa mauti;
adui yangu atasema, “Nimemshinda,”
nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.
Lakini ninategemea upendo wako usiokoma;
moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.
Nitamwimbia BWANA,
kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.
Copyright information for Neno