Psalms 130

Kuomba Msaada

(Wimbo Wa Kwenda Juu)

Kutoka katika vilindi ninakulilia, Ee BWANA,
Ee BWANA, sikia sauti yangu.
Masikio yako na yawe masikivu
kwa kilio changu unihurumie.
Kama wewe, Ee BWANA,
ungeweka kumbukumbu ya dhambi,
Ee BWANA, ni nani
angeliweza kusimama?
Lakini kwako kuna msamaha,
kwa hiyo wewe unaogopwa.
Namngojea BWANA, nafsi yangu inangojea,
katika neno lake naweka tumaini langu.
Nafsi yangu inamngojea Bwana
kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,
naam, kuliko walinzi
waingojeavyo asubuhi.
Ee Israeli, mtumaini BWANA,
maana kwa BWANA kuna upendo usiokoma,
na kwake kuna ukombozi kamili.
Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli
kutoka katika dhambi zao zote.
Copyright information for Neno