Psalms 133

Sifa Za Pendo La Undugu

(Wimbo Wa Kwenda Juu. Wa Daudi)

Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza
wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!
Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,
yakitiririka kwenye ndevu,
yakitiririka kwenye ndevu za Aroni,
mpaka kwenye upindo wa mavazi yake.
Ni kama vile umande wa Hermoni
unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni.
Kwa maana huko ndiko BWANA
alikoamuru baraka yake,
naam, hata uzima milele.
Copyright information for Neno