Psalms 15

Kitu Mungu Anachotaka

(Zaburi Ya Daudi)

BWANA, ni nani awezaye kukaa
katika Hekalu lako?
Nani awezaye kuishi
katika mlima wako mtakatifu?
Ni yule aendaye pasipo mawaa,
anayetenda yaliyo haki,
asemaye kweli toka moyoni mwake
na hana masingizio ulimini mwake,
asiyemtenda jirani yake vibaya
na asiyemsingizia mwenzake,
ambaye humdharau mtu mbaya sana,
lakini huwaheshimu wale
ambao humwogopa BWANA,
yule atunzaye kiapo chake
hata kama anaumia.
Yeye akopeshaye fedha yake bila riba,
na hapokei rushwa
dhidi ya mtu asiye na hatia.
Mtu afanyaye haya
kamwe hatatikisika.
Copyright information for Neno