Psalms 30

Maombi Ya Shukrani

Utenzi Wa Kuweka Wakfu Hekalu (Zaburi Ya Daudi)

Nitakutukuza wewe, Ee BWANA,
kwa kuwa umeniinua
na hukuacha adui zangu
washangilie juu yangu.
Ee BWANA, Mungu wangu, nilikuita unisaidie
na wewe umeniponya.
Ee BWANA, umenitoa Kuzimu,
umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.
Mwimbieni BWANA, enyi watakatifu wake;
lisifuni jina lake takatifu,
kwa kumbukumbu la utakatifu wake.
Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,
bali upendo wake hudumu siku zote;
inawezekana kilio kikawepo usiku kucha,
lakini asubuhi kukawa na furaha.
Nilipofanikiwa nilisema,
“Sitatikiswa kamwe.”
Ee BWANA, uliponijalia,
uliuimarisha mlima wangu,
lakini ulipouficha uso wako nilifadhaika.
Kwako wewe, Ee BWANA, niliita,
kwa Bwana niliomba rehema:
“Kuna faida gani katika kuangamia kwangu?
Katika kushuka kwangu shimoni?
Je, mavumbi yatakusifu?
Je, yatatangaza uaminifu wako?
10 Ee BWANA, unisikie na kunihurumia,
Ee BWANA, uwe msaada wangu.”
11 Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza,
ulinivua nguo za gunia
ukanivika shangwe,
12 ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya.
Ee BWANA Mungu wangu,
nitakushukuru milele.
Copyright information for Neno