Psalms 6

Sala Kwa Ajili Ya Msaada Wakati Wa Taabu

(Kwa Mwimbishaji: Kwa Ala Za Nyuzi Za Muziki. Mtindo Wa Sheminithi
6.0 Sheminithi ni mtajo mmojawapo katika lugha ya uimbaji
. Zaburi Ya Daudi)

1Ee BWANA, usinikemee katika hasira yako,
wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.
2Unirehemu BWANA,
kwa maana nimedhoofika;
Ee BWANA, uniponye,
kwa maana mifupa yangu
ina maumivu makali.
3Nafsi yangu ina uchungu mwingi.
Mpaka lini, Ee BWANA, mpaka lini?
4Geuka Ee BWANA, unikomboe,
uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.
5Hakuna mtu anayekukumbuka
akiwa amekufa.
Ni nani awezaye kukusifu
akiwa kuzimu?
6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni;
usiku kucha nafurikisha
kitanda changu kwa machozi;
nimelowesha viti vyangu vya fahari
kwa machozi.
7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,
yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.
8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,
kwa maana BWANA amesikia kulia kwangu.
9BWANA amesikia kilio changu kwa huruma,
BWANA amekubali sala yangu.
10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,
watarudi nyuma kwa aibu ya ghafula.
Copyright information for Neno