Psalms 97

Mungu Mtawala Mkuu

BWANA anatawala, nchi na ifurahi,
visiwa vyote vishangilie.
Mawingu na giza nene vinamzunguka,
haki na hukumu ndio msingi
wa kiti chake cha enzi.
Moto hutangulia mbele zake
na huteketeza adui zake pande zote.
Umeme wake wa radi humulika dunia,
nchi huona na kutetemeka.
Milima huyeyuka kama nta mbele za BWANA,
mbele za Bwana wa dunia yote.
Mbingu zinatangaza haki yake,
na mataifa yote huona utukufu wake.
Wote waabuduo sanamu waaibishwe,
wale wajisifiao sanamu:
mwabuduni yeye, enyi miungu yote!
Sayuni husikia na kushangilia,
vijiji vya Yuda vinafurahi
kwa sababu ya hukumu zako, Ee BWANA.
Kwa kuwa wewe, Ee BWANA,
ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote;
umetukuka sana juu ya miungu yote.
10 Wale wanaompenda BWANA na wauchukie uovu,
kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake
na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu.
11 Nuru huangaza wenye haki
na furaha kwa watu wanyofu wa moyo.
12 Furahini katika BWANA, ninyi mlio wenye haki,
lisifuni jina lake takatifu.
Copyright information for Neno