Song of Solomon 6

Marafiki 1Mpenzi wako amekwenda wapi,
yule mzuri kupita wanawake wote?
Mpenzi wako amegeukia njia ipi,
tupate kumtafuta pamoja nawe? Mpendwa
2Mpenzi wangu amekwenda bustanini mwake,
kwenye vitalu vya vikolezo,
kujilisha bustanini
na kukusanya yungiyungi.
3Mimi ni wake mpenzi wangu,
na mpenzi wangu ni wangu mimi;
huyu mwanaume hulisha katikati ya yungiyungi. Mpenzi
4Wewe ni mzuri, mpenzi wangu, kama Tirza,
upendezaye kama Yerusalemu,
umetukuka kama jeshi lenye bendera.
5Uyageuze macho yako mbali nami,
yananigharikisha.
Nywele zako ni kama kundi la mbuzi
wanaotelemka kutoka Gileadi.
6Meno yako ni kama kundi la kondoo
wanaotoka kuogeshwa.
Kila mmoja ana pacha lake,
hakuna hata mmojawapo aliye peke yake.
7Mashavu yako nyuma ya shela yako
ni kama vipande viwili vya komamanga.
8Panaweza kuwapo malkia sitini,
masuria themanini
na mabikira wasiohesabika;
9lakini hua wangu, mkamilifu wangu,
ni wa namna ya pekee,
binti pekee kwa mama yake,
kipenzi cha yeye aliyemzaa.
Wanawali walimwona na kumwita mbarikiwa;
malkia na masuria walimsifu. Marafiki
10Ni nani huyu atokeaye kama mapambazuko,
mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua,
ametukuka kama majeshi yenye bendera? Mpenzi
11Nilitelemka kwenye kichaka cha miti ya milozi
ili kutazama machipuko ya bondeni,
kuona kama mizabibu imechipua
au kama mikomamanga imechanua maua.
12Kabla sijang'amua,
shauku yangu iliniweka
katikati ya magari ya kifalme ya kukokotwa na farasi. Marafiki
13Rudi, rudi, Ee Mshulami;
rudi, rudi ili tupate kukutazama! Mpenzi
Kwa nini kumtazama Mshulami,
kama kutazama ngoma ya Mahanaimu
6.13 Mahanaimu hapa ina maana ya majeshi mawili
?
Copyright information for Neno