1 Chronicles 16:23-33


23 aMwimbieni Bwana dunia yote;
tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
24 bTangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,
matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.
25 cKwa kuwa Bwana ni mkuu,
mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote;
yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.
26 dKwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,
lakini Bwana aliziumba mbingu.
27Fahari na enzi viko mbele yake;
nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.
28 eMpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa,
mpeni Bwana utukufu na nguvu,
29mpeni Bwana utukufu
unaostahili jina lake.
Leteni sadaka na mje katika nyua zake;
mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.
30 fDunia yote na itetemeke mbele zake!
Ulimwengu ameuweka imara; hauwezi kusogezwa.
31 gMbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;
semeni katikati ya mataifa, “Bwana anatawala!”
32 hBahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;
mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo ndani yake.
33 iKisha miti ya msituni itaimba,
itaimba kwa furaha mbele za Bwana,
kwa maana anakuja kuihukumu dunia.
Copyright information for SwhNEN