1 Chronicles 16:8-22

8 aMshukuruni Bwana, liitieni jina lake;
wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.
9 bMwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa;
waambieni matendo yake yote ya ajabu.
10 cLishangilieni jina lake takatifu;
mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.
11 dMtafuteni Bwana na nguvu zake;
utafuteni uso wake siku zote.
12 eKumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,
miujiza yake na hukumu alizozitamka,
13enyi wazao wa Israeli mtumishi wake,
enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

14 fYeye ndiye Bwana Mungu wetu;
hukumu zake zimo duniani pote.
15Hulikumbuka agano lake milele,
neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
16 gagano alilolifanya na Abrahamu,
kiapo alichomwapia Isaki.
17 hAlilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,
kwa Israeli liwe agano la milele:
18 i“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani
kuwa sehemu utakayoirithi.”

19 jWalipokuwa wachache kwa idadi,
wachache sana na wageni ndani yake,
20walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,
kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
21 kHakuruhusu mtu yeyote awaonee;
kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
22 l“Msiwaguse niliowatia mafuta;
msiwadhuru manabii wangu.”
Copyright information for SwhNEN