1 Chronicles 25

Waimbaji

1 aDaudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii:

2Kutoka kwa wana wa Asafu walikuwa:
Zakuri, Yosefu, Nethania na Asarela. Wana wa Asafu walikuwa chini ya usimamizi wa Asafu, ambaye alitoa unabii chini ya usimamizi wa mfalme.
3 bWana wa Yeduthuni walikuwa sita:
Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia, na Matithia, nao walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao Yeduthuni, wao walikuwa wakitoa unabii wakitumia vinubi, wakimshukuru na kumtukuza Bwana.
4Wana wa Hemani walikuwa:
Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti na Romamti-Ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi.
5 cWote hawa walikuwa wana wa Hemani mwonaji wa mfalme. Aliwapata wana hawa kutokana na ahadi ya Mungu ili kumwinua. Mungu alimpa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.

6 dHawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la Bwana wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme. 7 ePamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa Bwana. Idadi yao walikuwa 288.
8
In order to format the table contained in this verse correctly, it has been necessary to move the content of some adjacent verses into it.
,
gVijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura.

 9 hKura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yosefu,

wanawe na jamaa zake,
12
Ya pili ikamwangukia Gedalia,

yeye na wanawe pamoja na jamaa zake,
12
 10Ya tatu ikamwangukia Zakuri,

wanawe na jamaa zake,
12
 11ya nne ikamwangukia Isri,
Isri jina lingine ni Seri.

wanawe na jamaa zake,
12
 12ya tano ikamwangukia Nethania,

wanawe na jamaa zake,
12
 13ya sita ikamwangukia Bukia,

wanawe na jamaa zake,
12
 14ya saba ikamwangukia Yesarela,
Yesarela jina lingine ni Asarela.

wanawe na jamaa zake,
12
 15ya nane ikamwangukia Yeshaya,

wanawe na jamaa zake,
12
 16ya tisa ikamwangukia Matania,

wanawe na jamaa zake,
12
 17ya kumi ikamwangukia Shimei,

wanawe na jamaa zake,
12
 18ya kumi na moja ikamwangukia Azareli,
Azareli jina lingine ni Uzieli.

wanawe na jamaa zake,
12
 19ya kumi na mbili ikamwangukia Hashabia,

wanawe na jamaa zake,
12
 20ya kumi na tatu ikamwangukia Shubaeli,

wanawe na jamaa zake,
12
 21ya kumi na nne ikamwangukia Matithia,

wanawe na jamaa zake,
12
 22ya kumi na tano ikamwangukia Yeremothi,

wanawe na jamaa zake,
12
 23Ya kumi na sita ikamwangukia Hanania,

wanawe na jamaa zake,
12
 24ya kumi na saba ikamwangukia Yoshbekasha,

wanawe na jamaa zake,
12
 25ya kumi na nane ikamwangukia Hanani,

wanawe na jamaa zake,
12
 26ya kumi na tisa ikamwangukia Malothi,

wanawe na jamaa zake,
12
 27ya ishirini ikamwangukia Eliatha,

wanawe na jamaa zake,
12
 28ya ishirini na moja ikamwangukia Hothiri,

wanawe na jamaa zake,
12
 29ya ishirini na mbili ikamwangukia Gidalti,

wanawe na jamaa zake,
12
 30ya ishirini na tatu ikamwangukia Mahaziothi,

wanawe na jamaa zake,
12
 31 lya ishirini na nne ikamwangukia Romamti-Ezeri,

wanawe na jamaa zake,
12.

31
Copyright information for SwhNEN