1 Chronicles 26:12-20
12Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa Bwana kama jamaa zao walivyokuwa nazo. 13 aKura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo.14 bKura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia. ▼
▼Shelemia jina lingine ni Meshelemia.
Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia. 15 dKura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe. 16 eKura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa.Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa: 17Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki, wanne upande wa kaskazini, wanne upande wa kusini, na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala. 18Kuhusu ukumbi kuelekea magharibi, kulikuwa na wanne barabarani na wawili kwenye ukumbi wenyewe.
19 fHii ndiyo iliyokuwa migawanyo ya mabawabu waliokuwa wazao wa Kora na wa Merari.
Watunza Hazina Na Maafisa Wengine
20 gKatika Walawi, Ahiya alikuwa mwangalizi wa hazina za nyumba ya Mungu na mwangalizi wa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.
Copyright information for
SwhNEN