1 Chronicles 26:13-19

13 aKura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo.

14 bKura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia.
Shelemia jina lingine ni Meshelemia.
Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia.
15 dKura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe. 16 eKura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa.

Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa:
17Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki, wanne upande wa kaskazini, wanne upande wa kusini, na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala. 18Kuhusu ukumbi kuelekea magharibi, kulikuwa na wanne barabarani na wawili kwenye ukumbi wenyewe.

19 fHii ndiyo iliyokuwa migawanyo ya mabawabu waliokuwa wazao wa Kora na wa Merari.

Copyright information for SwhNEN