1 Corinthians 12:4-11
4 aKuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. 5 bKuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule. 6 cKisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.7 dBasi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote. 8 eMaana mtu mmoja kwa Roho hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kwa Roho huyo huyo. 9 fMtu mwingine imani kwa huyo Roho na mwingine karama za kuponya kwa huyo Roho mmoja. 10 gKwa mwingine matendo ya miujiza, kwa mwingine unabii kwa mwingine kupambanua roho, kwa mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingine bado, tafsiri za lugha. 11 hHaya yote hufanywa na huyo huyo Roho mmoja, Roho naye humgawia kila mtu, kama apendavyo.
Copyright information for
SwhNEN