1 Kings 11:41-43
Kifo Cha Solomoni
(2 Nyakati 9:29-31)
41Kwa habari za matukio mengine ya utawala wa Solomoni, yote aliyoyafanya na hekima aliyoionyesha, je hayakuandikwa yote katika kitabu cha matendo cha Solomoni? 42Solomoni alitawala Israeli yote miaka arobaini, akiwa Yerusalemu. 43Kisha Solomoni akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa katika mji wa Daudi baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akawa mfalme baada yake.
Copyright information for
SwhNEN