1 Kings 9:11-14
11 aMfalme Solomoni akampa Hiramu mfalme wa Tiro miji ishirini katika Galilaya, kwa sababu Hiramu alikuwa amempatia mierezi yote, misunobari na dhahabu yote aliyohitaji. 12 bLakini Hiramu alipotoka Tiro kwenda kuiona ile miji ambayo Solomoni alikuwa amempa, hakupendezwa nayo. 13 cHiramu akauliza, “Hii ni miji ya namna gani uliyonipa, ndugu yangu?”Naye akaiita nchi ya Kabul, ▼
▼Kabul maana yake isiyofaa kitu.
jina lililoko hadi leo. 14 eBasi Hiramu alikuwa amempelekea mfalme talanta 120 ▼▼Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5.
za dhahabu.
Copyright information for
SwhNEN