2 Samuel 2:1-4
Daudi Atiwa Mafuta Kuwa Mfalme Wa Yuda
1 aIkawa baada ya mambo haya, Daudi akamuuliza Bwana, “Je, nipande kwenda katika mojawapo ya miji ya Yuda?”Bwana akasema, “Panda.”
Daudi akauliza, “Je, niende wapi?”
Bwana akajibu, “Nenda Hebroni.”
2 bBasi Daudi akakwea kwenda huko pamoja na wake zake wawili, Ahinoamu wa Yezreeli na Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. 3 cPia Daudi akawachukua watu waliokuwa pamoja naye, kila mmoja na jamaa yake, nao wakaishi huko Hebroni na miji yake. 4 dNdipo watu wa Yuda wakaja Hebroni, huko wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya nyumba ya Yuda.
Daudi alipoambiwa kuwa ni watu wa Yabeshi-Gileadi waliomzika Sauli,
Copyright information for
SwhNEN