Acts 2:33-38
33 aBasi ikiwa yeye ametukuzwa kwa mkono wa kuume wa Mungu, amepokea kutoka kwa Baba ahadi ya Roho Mtakatifu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia. 34 bKwa kuwa Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini anasema,“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
35 chadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako.” ’
36 d“Kwa hiyo Israeli wote na wajue jambo hili kwa uhakika kwamba: Mungu amemfanya huyu Yesu, ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa Bwana na Kristo.”
Waumini Waongezeka
37 eWatu waliposikia maneno haya yakawachoma mioyo yao, wakawauliza Petro na wale mitume wengine, “Ndugu zetu tufanye nini?”38 fPetro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Copyright information for
SwhNEN