Amos 1:6-8
6 aHili ndilo asemalo Bwana:“Kwa dhambi tatu za Gaza,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima
na kuwauza kwa Edomu,
7 bnitatuma moto juu ya kuta za Gaza
ambao utateketeza ngome zake.
8 cNitamwangamiza mfalme wa Ashdodi
na yeye aishikaye fimbo ya utawala katika Ashkeloni.
Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni,
hadi Mfilisti wa mwisho atakapokufa,”
asema Bwana Mwenyezi.
Copyright information for
SwhNEN