Amos 5:11-12


11 aMnamgandamiza maskini
na kumlazimisha awape nafaka.
Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari,
hamtaishi ndani yake;
ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu,
hamtakunywa divai yake.
12 bKwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu
na ukubwa wa dhambi zenu.

Mmewaonea wenye haki na kupokea rushwa
na kuzuia haki ya maskini mahakamani.
Copyright information for SwhNEN