Amos 5:16-23

16 aKwa hiyo hili ndilo Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, asemalo:

“Kutakuwepo maombolezo katika barabara zote
na vilio vya uchungu katika njia kuu zote.
Wakulima wataitwa kuja kulia,
na waombolezaji waje kuomboleza.
17 bKutakuwepo kuomboleza katika mashamba yote ya mizabibu,
kwa kuwa nitapita katikati yenu,”
asema Bwana.

Siku Ya Bwana

18 cOle wenu ninyi mnaoitamani
siku ya Bwana!
Kwa nini mnaitamani siku ya Bwana?
Siku hiyo itakuwa giza, si nuru.
19 dItakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simba
kumbe akakutana na dubu,
kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwake
na kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta,
kumbe akaumwa na nyoka.
20 eJe, siku ya Bwana haitakuwa giza, na si nuru:
giza nene, bila mwonzi wa mwanga?

21 f“Ninachukia, ninazidharau sikukuu zenu za dini;
siwezi kuvumilia makusanyiko yenu.
22 gHata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za nafaka,
sitazikubali.
Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani,
sitazitambua.
23Niondoleeni kelele za nyimbo zenu!
Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu.
Copyright information for SwhNEN