Amos 5:18-20
Siku Ya Bwana
18 aOle wenu ninyi mnaoitamanisiku ya Bwana!
Kwa nini mnaitamani siku ya Bwana?
Siku hiyo itakuwa giza, si nuru.
19 bItakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simba
kumbe akakutana na dubu,
kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwake
na kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta,
kumbe akaumwa na nyoka.
20 cJe, siku ya Bwana haitakuwa giza, na si nuru:
giza nene, bila mwonzi wa mwanga?
Copyright information for
SwhNEN