Amos 5:2-5
2 a“Bikira Israeli ameanguka,kamwe hatainuka tena,
ameachwa pweke katika nchi yake,
hakuna yeyote wa kumwinua.”
3 bHili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“Wakati mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani kwa ajili ya Israeli,
mia moja tu watarudi;
wakati mji utakapopeleka mia moja,
kumi tu ndio watarudi hai.”
4 cHili ndilo Bwana asemalo kwa nyumba ya Israeli:
“Nitafuteni mpate kuishi;
5 dmsitafute Betheli,
msiende Gilgali,
msisafiri kwenda Beer-Sheba.
Kwa maana kwa hakika Gilgali itakwenda uhamishoni,
na Betheli itafanywa kuwa si kitu.” ▼
▼Yaani Aveni kwa Kiebrania, kumaanisha Beth-Aveni, jina lingine la Betheli kwa dhihaka.
Copyright information for
SwhNEN