Deuteronomy 1:26-33

Uasi Dhidi Ya Bwana

(Hesabu 14:20-45)

26 aLakini hamkuwa tayari kukwea, mkaasi dhidi ya amri ya Bwana Mungu wenu. 27 bMkanungʼunika ndani ya mahema yenu na kusema, “Bwana anatuchukia, kwa hiyo alitutoa Misri ili kututia mikononi mwa Waamori kutuangamiza. 28 cTwende wapi? Ndugu zetu wametufanya kufa moyo. Wanasema, ‘Watu wa huko wana nguvu zaidi na ni warefu kuliko sisi tulivyo; miji ni mikubwa, yenye kuta zilizofika juu angani. Zaidi ya hayo, tumewaona Waanaki huko.’ ”

29 dNdipo nikawaambia, “Msihofu, wala msiwaogope. 30 eBwana Mungu wenu anayewatangulia, atawapigania, kama alivyofanya kwa ajili yenu huko Misri, mbele ya macho yenu hasa, 31 fna pia huko jangwani. Huko mliona jinsi Bwana Mungu wenu alivyowachukua, kama baba amchukuavyo mwanawe, katika njia yote mliyoiendea mpaka mkafika mahali hapa.”

32 gPamoja na hili, hamkumtegemea Bwana Mungu wenu, 33 hambaye aliwatangulia katika safari yenu, kwa moto usiku na kwa wingu mchana, kuwatafutia mahali penu pa kupiga kambi na kuwaonyesha njia mtakayoiendea.

Copyright information for SwhNEN