c Law 26:16; Yer 42:18; Mal 2:2; 3:9; 4:6; Za 39:11; 76:6; 80:16; Isa 17:13; 51:20; 54:9; 66:15; Eze 5:15; Kum 4:26; Kut 32:22
Deuteronomy 28:15-24
Laana Kwa Kutokutii
(Walawi 26:14-46)
15 aHata hivyo, kama hutamtii Bwana Mungu wako na kuzishika kwa bidii amri zake zote na maagizo ninayokupa leo, laana hizi zote zitakuja juu yako na kukupata:16Utalaaniwa mjini na utalaaniwa mashambani.
17Kapu lako na chombo chako cha kukandia kitalaaniwa.
18 bUzao wa tumbo lako utalaaniwa, mazao ya ardhi yako, ndama wa makundi yako ya ngʼombe na wana-kondoo wa makundi yako.
19Utalaaniwa uingiapo na utokapo.
20 c Bwana ataleta laana juu yako, fadhaa na kukaripiwa katika kila kitu unachokigusa kwa mkono wako, mpaka uwe umeharibiwa na kuangamizwa ghafula kwa ajili ya maovu uliyoyafanya kwa kumwacha yeye. 21 dBwana atakupiga kwa magonjwa mpaka akuangamize kutoka nchi unayoingia kuimiliki. 22 eBwana atakupiga kwa magonjwa ya kudhoofisha, kwa homa na kuwashwa, hari na kwa ukame, kutu na kuwa na uchungu ambavyo vitakupiga mpaka uangamie.
23 fAnga juu yako itakuwa shaba, na ardhi chini yako itakuwa chuma. 24 gBwana atafanya mvua ya nchi yako kuwa mavumbi na mchanga; vitakujia kutoka angani mpaka uangamie.
Copyright information for
SwhNEN