‏ Deuteronomy 28:3-6

3 aUtabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani.

4 bUtabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ngʼombe, na wana-kondoo wa makundi yako.

5Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa.

6 cUtabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo.

Copyright information for SwhNEN