Deuteronomy 6:4-9

4 aSikia, ee Israeli: Bwana Mungu wako, Bwana ni mmoja. 5 bMpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 cAmri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. 7 dWafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. 8 eZifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako. 9 fZiandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.

Copyright information for SwhNEN