Exodus 1:6-10

6 aBasi Yosefu na kaka zake wote na kizazi kile chote walikufa, 7 blakini Waisraeli walikuwa wamezaana na kuongezeka sana, idadi yao ikawa kubwa mno, kwa hiyo wakaijaza nchi.

8 cKisha mfalme mpya ambaye hakufahamu habari za Yosefu akatawala Misri. 9 dAkawaambia watu wake, “Tazameni, Waisraeli wamekuwa wengi mno kwa idadi kutuliko sisi. 10 eNjooni, ni lazima tuwashughulikie kwa uangalifu, la sivyo watazidi kuwa wengi zaidi, na ikiwa patatokea vita, watajiunga na adui zetu kupigana dhidi yetu na kuondoka katika nchi hii.”

Copyright information for SwhNEN